20 Agosti 2025 - 19:28
Idadi ya Mashahidi Gaza Yaongezeka Hadi 62,122

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa baada ya kuuwawa kwa watu wengine 58 kutokana na mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni, idadi ya jumla ya mashahidi imefikia 62,122.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- idadi ya watu waliojeruhiwa katika mashambulizi ya jeshi la Kizayuni tangu kuanza kwa vita katika Ukanda wa Gaza sasa imefikia 156,758.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa tangu tarehe 18 Machi 2025, katika wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Gaza, watu 10,576 wameuawa shahidi na wengine 44,717 wamejeruhiwa.

Aidha, maelfu ya watu bado hawajulikani walipo na wameripotiwa kufunikwa chini ya vifusi.

Katika vituo vya kugawa misaada, ndani ya masaa 24 yaliyopita, watu 22 wameuawa shahidi na wengine 49 kujeruhiwa, na hivyo kufanya idadi ya Wapalestina waliouawa katika maeneo hayo kufikia 2,018, huku waliojeruhiwa wakifikia 14,947.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha